TAHADHARI NA AINA HIZI ZA PETE

Watu wengi wamekuwa wakipendelea sana kuva pete zenye stone nyingi ndogo ndogo pembeni (kama hiyo hapo juu), ila baada ya muda huwa kero kwa mvaaji na kuichukia kabisa pete yake. Nikweli pete za aina hii ni nzuri sana machoni mwa watu na zinapendeza sana mtu akivaa mana zinaleta taswira ya mvuto fulani na kumfanya mvaaji ajisikie amependeza. Ila changamoto ya pete hizi ikianza huwa ni kero sana kwa mvaaji kwani ni rahisi kuichoka, Baada ya muda kupita hizo stone za pembeni huwa zinatoka(zinachomoka) moja moja baada ya muda huifanya pete kuwa na vishimo vingi vidogo vidogo na kuondosha uzuri au urembo wa pete. pia ni changamoto kwenye kuzikosha pete kama hizo kwani zinahitaji tahadhari ya hali ya juu, kwani unaweza kukosana na muoshaji (sonara) kuwa amekuharibia pete yako kumbe ni hali tu ya kudondoka ya hizo stone za pembeni ndogo ndogo wakati ali...