JINSI YA KUJUA DHAHABU(GOLD) HALISI NA KUEPUKANA NA MATAPELI

Watu wengi wanatapeliwa kwa sababu ya kukosekana kwa vipimo sahihi vinavyoweza kubainisha kama bidhaa waliouziwa ni bandia ama ni halisi. Kwa miaka kadhaa baddhi ya watu wamekuwa wakitapeliwa kwa kuuziwa bidhaa bandia za dhahabu au zilizo chini ya kiwango. Matapeleli hao wamekuwa wakiuza bidhaa za chuma au bati mfano kama pete kwa kuzipaka kiwango kidogo cha nakshi za dhahabu au rangi ya dhahabu wakinadi kuwa zimetengenezwa kwa madini ya dhahabu halisi. Mbali na matapeli wa mtaani na katika masoko mbalimbali, pia wapo baadhi ya wafanya biashara ambao wasio waaminifu wanaofanya udanganyifu kwa kupunguza kiwango cha dhahabu katika bidhaa husika, ili kujipatia fedha(pesa) nyingi katika kiasi kidogo cha madini. Hata hivyo, kwa kutumia njia za kawaida sana upo uwezekano wa kugundua iwapo bidhaa ya dhahabu uliou...